Monday, April 17, 2017

Park Geun-hye: Aliyekuwa Rais wa Korea Kusini ashtakiwa kuhusu rushwa



Rais wa South Korea aliyeondolewa mamlakani Park Geun-hye ameshtakiwa rasmi kuhusiana na kashfa ya rushwa iliyopelekea kung'atuliwa kwake uongozini.

Viongozi wa mashtaka wanasema kuwa mashtaka yanayomkabili ni kupokea hongo, utumizi mbaya wa mamlaka, na kudukua siri za serikali.

Park, 65, ambaye yupo kizuizini, ameshtakiwa kwa kumruhusu rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil kutoza fedha kampuni kadha kuu ili wapendelewe kisiasa.

Wanawake wote wawili walikana mashtaka.

Bi Park alitolewa ofisini mwezi uliopita.

Alipoteza kinga yake na kutolewa mamlakani baada ya mahakama ya kikatiba kuidhinisha uamuzi ya bunge kumng'atua uongozini.

Mkuu wa Samsung akamatwa Korea Kusini
Rais wa zamani Korea Kusini akamatwa
Rais wa Korea Kusini alihusika kwenye ufisadi

Bi Choi anatuhumiwa kutumia uhusiano wake wa kirais ili kuweka shinikizo kwa kampuni kutoa mamilioni ya madola katika michango kwa mashirika yasiyo ya serikali ambayo anayashikilia.

Bi Park anadaiwa kuhusika binafsi katika masuala hayo, na kumpa Bi Choi ruhusa isiyokubalika kupata nyaraka rasmi.

Kati ya kampuni hizo, ni kampuni kubwa nchini humo, Samsung.

Kaimu Kiongozi wake Lee Jae-yong na Bi Choi wamewekwa pamoja kizuizini huku Bi park akingojea kesi dhidi yake ianze.

Mwenyekiti wa kampuni ya Lotte Shin Dong-bin alishtakiwa kutoa rushwa Jumatatu, lakini viongozi wa mashtaka hawakumweka kizuizini.

Wote wawili, Samsung na Lotte wamekanusha mashtaka dhidi yao.

Hwang Kyo-ahn, ambaye ni mwaminifu kwake Bi Park, ndiye kaimu rais huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika tarehe 9 mwezi Mei.

No comments:

Post a Comment