Monday, April 17, 2017

Bank ya Exim yajipanga kutanua wigo wa utoaji huduma katika ukanda wa Afrika Mashariki


Ikiwa ni miaka 20 tangu kuanza kwake kutoa huduma kwa wananchi katika masuala ya kifedha, Benki ya Exim imejipanga kutanua wigo wake wa kibiashara wa utoaji huduma katika nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika Mashariki.

Sambamba na Tanzania, tayari benki hiyo imeweza kupeleka huduma zake katika nchi za Comoro, Djibout na Uganda huku bado ikiendelea kufikiria kutanua wigo wake zaidi na zaidi. Mipango hiyo imeelezwa na George Shumbusho, Mkuu wa Hazina wa Exim Bank.

Shumbusho anasema “Miaka 20 ya mafanikio katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, kwa maana ya Tanzania, Comoro na Djibout na Uganda, bado tunafikiri kuendelea kutanua mipaka yetu kutokana na mahitaji ya soko”.

Mbali na kutanua wigo wa utoaji huduma kwa wateja kulingana na uhitaji wa soko, Shumbusho anasema kuwa benki hiyo imeweka mkazo katika kutoa huduma bora zenye kuweka mbele maslahi ya mteja.

“Tunajikita zaidi katika kuhakikisha mteja ndio sehemu ya kati ya mtazamo wetu. Uwekezaji wetu unalenga katika kuhakikisha mahitaji ya kibenki ya mteja wetu yanapata suluhisho sahihi ndani ya Bank hii”, Anaongezea George Shumbusho.

Hii ina maana kuwa, licha ya Exim Bank kujipanga katika kuhakikisha inatanua wigo wa huduma kwa wateja wa ndani na nje ya nchi, lakini pia wanajipanga katika kutoa huduma bora kwa wateja wao hao ambao ndio kitovu kikuu cha biashara yao.

No comments:

Post a Comment